
Razak Abalora golikipa wa zamani wa AZAM
Abalora mwenye umri wa miaka 24 ambaye kwa sasa anacheza klabu ya Asante Kotoko ya nyumbani kwao Ghana inayoshiriki ligi kuu, amekuwa miongoni mwa wachezaji 29 walioitwa na kocha mzawa Charles Kwabla' Ck' Akonnor,
Abalora alijiunga na Azam akitokea timu ya Wafu nyumbani kwao mwaka 2017 na kudumu kwa miak a 4 ,alianza kuitwa timu ya taifa ya Ghana akiwa bado Azam hali inayotoa tafsiri kukua kwa ligi ya Tanzania kwa sababu Wagahana wanaocheza soka wapo wengi na wamesambaa sana duniani.
Hata katika kikosi kilichoitwa, kuna wachezaji 9 wanaocheza ndani na 20 wanaocheza nje ya nchi akiwemo mshambuliaji wao bora wa zamani aliyekipiga katika vilabu mbalimbali vya Uhispania kama Villareal, Espanyo Granada na Alaves, Mubaraka Wakaso ambaye kwa sasa anacheza china klabu ya Jiangsu Suning.
Katika uteuzi uliyopita ulimjumuisha mchezaji mwingine kutoka Azam Yakubu Mohamed alishiriki mechi mbili za kirafiki., pia mshambuliaji wa Pyramids aliyeng'ara katika mchezo dhidi ya Namungo katika mchezo wa shirikisho John Antwi pamoja na Fatawu Issahaku mchezaji bora wa AFCON ya vijana U-20 yaliyomalizika majuzi nchini Cameroon.