Jumatano , 24th Mar , 2021

klabu ya Real Madrid ya Hispania imemuweka mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane kama chaguao la kwanza kwenye orodha ya wachezaji inayowawania katika dirisha la usajili la majira ya joto linalofata wakiaamini ni rahisi kukamilisha usajili wa mchezaji huyo kuliko ule wa Mbappe na Halaand.

Harry Kane

Madrid wanahitaji kusajili mshambuliaji wa kiwango cha Dunia katika harakati za kuboresha kikosi hicho kwenye safu ya ushambuliaji kuelekea msimu ujao wa 2021-22, na kwenye orodha ya wachezaji wanaotajwa kuwaniwa ni mshambjuliaji wa Tottenham ya England Harry Kane, Kylian Mbappe wa PSG ya Ufaransa na Erling Haaland wa Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Ripoti kutoka nchini Ujerumani zinaripoti kuwa mabingwa hao wa kihistoria wa ulaya kwa sasa kipaumbele chao ni kumsajili Harry Kane kwani anaonekana ndio mchezaji wanaoweza kumpata kiurahisi ukilinganisha na Mbappe na Halaanda.

Mbappe mwenye umri wa maiak 22, anasimamiwa na wazazi wake kwenye swala la mikataba hivyo wanaamini kuna ugumu watakutana nao, wakati Halaand mwenye miaka 20 wakala wake ni Mino Raiola ambaye anatajwa kuwa anahitaji pesa nyingi sana kwenye makubaliano ya kumuuza mchezaji huyo.

Harry Kane Raia wa England mwenye umri wa miaka 27 ameshaifungia Tottenham mabao 215 kwenye michezo 377, inatajwa nae yupo tayari kuondoka Spurs endapo kama kikosi hicho hakitapata nafasi ya kushiriki mashindano ya klabu bingwa ulaya msimu ujao na kama kitamaliza msimu huu bila kushinda kombe lolote, na mkatab wake na klabu hiyo unamalizika mwaka 2024.

Hivyo inaonekana hakutakuwa na ugumu kwa Real Madrid  kufanya makubaliano na Harry Kane ambayo kwa umri wake amekuwa akitajwa kuwa anahitaji kushinda mataji makubwa, na kwa mwenendo wa Spurs inaonekana ni ngumu kushinda mataji akaiwa na kikosi hicho.