Jumatano , 20th Apr , 2022

Waziri wa Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Hassani Njama Hassani kupisha uchunguzi, kutokana na kushindwa  kuutekeleza maagizo ya Waziri aliyoyatoa wakati wa ziar

Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa katika ziara ya waziri alibaini upotevu mkubwa wa fedha za miradi na matumizi yasiyo sahihi ya shilingi bilioni 231.84 katika shule ya sekondari ya kumbukumbu ya Moringe Sokoine zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula

Waziri Bashungwa alimuagiza mkurugenzi huyo kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika upotevu wa fedha hizo, ambapo hadi kufikia leo Aprili 20/2022 hakuna mtumishi aliyechukuliwa hatua