Jumatano , 20th Apr , 2022

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linamshikilia dereva wa lori, aliyesababisha ajali na kupelekea vifo vya watu sita na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kuigonga Toyota Noah, katika eneo la Alkatani, Kata ya Sepeko, Tarafa ya Kisongo wilaya ya Monduli mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo, akiwa eneo la ajali

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 20, 2022, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo, na kusema kwamba Toyota Noah yenye namba za usajili T.189 DFY ilikuwa ikitokea Arusha mjini kwenda Karatu na lori lenye namba za usajili T.250 CAA lilikuwa linatokea Makuyuni kwenda Arusha mjini.

ACP Masejo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva amabapo alishindwa kulimudu gari hilo na kuhamia upande mwingine wa barabara na kusabisha kugonga gari hilo aina ya toyota Noah hiyo.

Kamanda Masejo amesema kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kufamu majina halisi ya abiria waliofariki katika ajali hiyo na amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya mkoa wa Arusha Mount Meru kutambua miili ya marehemu.