Jumapili , 9th Oct , 2022

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtandao wa maadili juu ya virusi vya UKIMWI nchini Kenya   (KELIN), Kliniki za wagonjwa wa VVU zipo kwenye maeneo ya wazi katika hosptali mbalimbali jambo linalosababisha kukosa usiri kwa waathirika.  

Waathirika wengi wanalalamika kuitwa majina yao kwa sauti na watoa huduma wakati wa kuwapatia dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo. 

Utafiti uliofanyika katika majimbo manne kwenye kautini ya  Kisumu ulihusisha wanawake 102 wenye umri kati ya miaka 16 na 34.   

Taarifa zimeonyehsa kwamba watoa huduma hawana mafunzo ya kutunza siri za waathuirika.  Baadhi ya wanawake wanasema kwamba walikua wakiulizwa hali zao za VVU mbele ya wagonjwa wengine.