Ijumaa , 4th Nov , 2022

Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani nchini Ramadhan Ng’anzi amesema atawachukulia hatua za kisheria askari wa Kikosi hicho watakaobainika kuomba Rushwa na kuwaonea watumiaji wa barabara

Ameyasema hayo leo akiwa Jijini mwanza punde baada ya kufanyika makabidhiano ya mkoa huo kwa  mkuu mpya wa Jeshi la Polisi jijini humo Wilibrod Mtafungwa yaliyofanyika katika kata ya Mabatini Wilaya Nyamagana mkoani humo ndipo akakemea vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya askari wa barabarani

‘Sitapenda kuona askari wetu wanawaonea watu wanaotumia barabara zetu kwa kuwabambikia kesi au kuwapa makosa ambayo hawakufanya lakini ningependa kuona kikosi kinafanya kazi kwa weledi wa hali ya juu na kuzingatia haki na weledi wa hali ya juu na kuondoa vitendo vya tuhuma za rushwa’

Kwa upande wake Mkuu wa jeshi la polisi mkoani Mwanza Wilibrod Mutafungwa amesema atahakikisha anayaendeleza yaliyofanywa na kamanda Ng’anzi katika mkoa huo ikiwa ni pamoja na kujenga umoja na uadlifu mkoani humo.
‘Yale mazuri ambayo Afande ameyataja hapa hatuna sababu ya kusita tunachofanya ni kusukuma mbele ili tuwe na mafanikio Zaidi nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha nawaunganisha pamoja’