Jumanne , 22nd Nov , 2022

Mamlaka katika jimbo la Kaskazini Magharibi mwa Nigeria la Zamfara zinasema watu wasiopungua 130 wametekwa nyara na watu wenye silaha katika mfululizo wa mashambulizi katika maeneo mawili tofauti ya jimbo hilo.

Kamishna wa habari Ibrahim Dosara ameiambia amesema kwamba juhudi zinaendelea kuwaokoa mateka hao.Utekaji nyara wa watu wengi ulitokea mwishoni mwa wiki wakati watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki walipovamia vijiji kadhaa.

Ripoti zinasema waathiriwa ni pamoja na wanawake na watoto  ambapo wengine walikamatwa wakati wakifanya kazi katika mashamba.

Ukiwa ni ni msimu wa uvunaji nchini Nigeria na magenge ya utekaji nyara yenye silaha hivi karibuni yamewalenga wafanyakazi wa mashamba katika eneo hilo.

Katika baadhi ya maeneo kaskazini magharibi mwa nchi, watekaji nyara wameweka ushuru kwa wakulima kama sharti la kuwaruhusu kuvuna mazao yao bila kizuizi.

Ukosefu wa usalama ni mojawapo ya masuala muhimu ya kampeni kabla ya uchaguzi wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika Februari mwaka ujao  wakati mrithi wa Rais Muhammadu Buhari atakapochaguliwa.