
Baba wa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 30 alisimulia jinsi alivyopigiwa simu na mwanae kuomba msaada wakati amefukiwa na maporomoko hayo , lakini hakuweza kumuokoa.
Mwili wa binti huyo ni kati ya miili mitano iliyopatikana na waokoaji, lakini watu wasiopungua tisa bado hawajulikani walipo katika kisiwa hicho cha Naples.
Mlipuko wa tope na vifusi uliharibu nyumba na kuvuta magari baharini.
Hayo yanafuatia siku kadhaa za mvua isiyokoma kusini mwa Italia, lakini sasa hali ya hewa imepungua, kiwango cha uharibifu kinafanyiwa tathmini.
Zaidi ya wazima moto 100, pamoja na wapiga mbizi na vitengo vya ardhini, wamepelekwa Ischia kujaribu kusafisha mitaa iliyojaa vifusi.