Jumanne , 17th Jan , 2023

Kiongozi wa chama cha Roots nchini Kenya Profesa George Wajackoyah, amemuomba Rais William Ruto, kuruhusu polisi na wanajeshi wanawake ambao ni waislamu kuvaa vazi la hijab wanapokuwa kwenye majukumu yao.

Profesa George Wajackoyah

Wajackoyah ametoa ombi hilo akitaka maafisa hao wa polisi waruhusiwe kuvaa hijab chini ya kofia zao ili kuendana na imani yao ya Kiislamu hata wakiwa kazini.

"Ninataka wanawake wa Kiislamu ambao wapo kwenye vikosi vya polisi na jeshi wavae ile nguo yao ya Kiislamu inayofunika kichwa, (Hijab) tunataka Uislamu uonekane kila mahali nchini Kenya," amesema Profesa Wajackoyah

Aidha Profesa Wajackoyah pia ametoa rai kwa serikali kuwatengea mapumziko ya kila wiki waumini hao ili wapate muda wa kuabudu.