Jumatatu , 8th Mei , 2023

Mtoto wa miaka minne mkazi wa mtaa wa Mwatulole Halmashauri ya Mji Geita ambaye jina lake limehifadhiwa amelawitiwa na wachungaji wawili wa ng'ombe wa nyumbani kwao kwa kumlaghai watampa pipi watakaporejea nyumbani.

Mama akiwa na mtoto wake aliyelawitiwa

Akielezea alivyofanyiwa ukatili mhanga wa tukio hilo anasema walikuwa wameenda kuchunga ng'ombe wakiwa malishoni wachungaji hao walimvua nguo na kumwambia watamnunulia pipi wakirudi nyumbani.

Akisimulia mama wa mtoto huyo amesema kuwa, "Kalipofika katoto kakavua gambuti kalivyovua kakaenda chooni, kametoka kakaingia ndani kulala mimi nilikuwa napikapika maana ilikuwa mida ya saa moja, nimemaliza kupika nikawaambia wenzie mwiteni fulani aje tule wakasema amelala, muamsheni yeye akatoka tena akaenda chooni, nikasema umekuwaje akasema mama tumbo linauma nikahisi labda ni mchafuko tu wa tumbo,"

Aidha mama huyo ameongeza kuwa, "Nikachukua ka fragile nikampa Ila akakataa hata kula akaenda tena kulala, nilivyombeba akawa analia tu mama tumbo nataka niende chooni sasa ikabidi nichukue poti nikamkalisha kwenye poti ili nione hicho kinyesi ni cha aina gani ambacho analia, kwakweli kile kinyesi nilivyokiona nilistuka maana hakikuwa cha kawaida ilikuwa ni uchafu uchafu mweupe umechanganyikana na damu, nikamuuliza umekuwaje Mama naumia huko kuna kidonda,".

Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mwatulole wamekiri kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wao.

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali teule ya  rufaa ya mkoa wa Geita Dokta Pascalate Mjuni, amekiri mtoto kupokelewa usiku wa Aprili 29 na kupatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa kurudi nyumbani.