
Yanga na Muramo kuamuliwa VAR.
Akitoa taarifa hiyo Kaimu meneja wa uwanja wa Mkapa , Milinde Mahona kuwa maandalizi yanakwenda vizuri na wataalamu hao hawajapata changamoto yoyote katika ufungaji wa vifaa hivyo kila kitu kinakwenda Vizuri.
'' Maandalizi yanakwenda vyema kwa kila mtu kuwajibika kwenye nafasi hivyo, mashabiki wajitokeze kutoa hamasa kwa timu yao '' Mahona Kaimu Meneja Uwanja Benjamin Mkapa
Pia kaimu huyo ametoa rai kwa mashabiki kuwa wazalendo pindi wanapokwenda uwanjani hususani kutunza miundombinu ya uwanja huku hatua kali zaidi zitachukuliwa kwa wale wenye tabia ya kuvunja au kuharibu miundombinu ya uwanja.
Kwa upande mwingine Afisa habari wa Yanga Ally Kamwe amesema ni kweli wamepokea barua kutoka Shirikisho la soka barani Afrika ya kwa kupigwa faini ya jumla ya Dola 35,000 na Caf ambayo ni zaidi ya Sh 82 milioni kwa makosa mbalimbali yanayodaiwa kufanywa katika mechi yao ya robo fainali kati yao na Rivers United ya Nigeria.
''Uongozi wa Yanga umekutana na leo umekata rufaa kupiga maamuzi hayo hivyo tunawasubiri nini ambayo watajibiwa na CAF ''amesema Kamwe Afisa habari Yanga