Tanzania yapokea mkopo kutoka AfDB

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Patricia Laverley, wakisaini mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani Milioni 125.2, sawa na sh. bilioni 289.34 kwa ajili ya Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Afisa Sheria Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Paulina Fungameza.
Wakazi wa jiji la Dodoma na Wilaya za Bahi, Chemba na Chamwino wanatarajia kuondokana na adha ya maji hivi karibuni baada ya Benki ya Maendeleo ya Afrika – AfDB, kutoa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 125. 2, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 289.34 kwa ajili ya ut