"Kuhusu wabunge 19 hatuiingilii Mahakama" - Spika
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, amesema hawezi kutangaza kuwa nafasi 19 za wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA ziko wazi, hadi hapo Mahakama itakapotoa uamuzi kwani Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa Mahakama.