Polisi wapewa mafunzo juu ya kuhudumia watalii
Jeshi la Polisi nchini limeanzisha kitengo maalumu cha utalii na diplomasia ambacho kipo kwa ajili ya kuwahudumia watalii na wanadiplomasia wanaofika nchini na kwamba limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama baada ya Rais Samia kuzindua filamu ya The Royal Tour kwa lengo la kukuza utalii.