Siasa safi ni uzalendo na utu - Shaka
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka, amewahakikishia Watanzania kwamba chama hicho kitaendelea kuisimamia serikali izidi kuimarisha uhuru wa maoni, misingi ya haki na demokrasia ili kujenga Taifa lenye upendo, umoja, amani na mshikamano wakati wote.

