Mabasi ya Mwendokasi yatumie gesi - Jafo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo, ameshauri ununuzi wa magari mapya ya mwendokasi uzingatie usafi wa mazingira na ikiwezekana yanunuliwe mabasi yanayotumia nishati ya gesi.

