Hamilton arejea Mercedes
Lewis Hamilton amerejea kwenye timu yake ya Mercedes wiki hii kujiandaa na msimu mpya wa langalanga ambapo hapo awali majaaliwa ya ushiriki wake ulikuwa ukitiliwa shaka kutokana changamoto zilizojitokeza kwenye mashindano ya kumpata bingwa kwa mwaka 2021(Abu Dhabi Grand Prix 2021).

