Wachezaji Yanga wapewa mapumziko ya siku 1
Timu ya wananchi na vinara wa Ligi kuu Tanzania bara Yanga SC imewapa mapumziko ya siku 1 wachezaji wake baada ya kikosi hicho kurejea kutoka jijini Arusha jana na wanatarajiwa kurejea tena kambini kesho Jumatano mchana tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Mbao FC.

