Bilionea Bezos aruka angani na roketi yake
Tajiri mkubwa duniani na Muanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Amazon Jeff Bezos amefanikiwa kwenda kwenye anga la juu zaidi na kurudi duniani ndani ya dakika 11 kwa kutumia roketi iliyotengenezwa na kampuni yake akivunja rekodi iliyowekwa na Bilionea Richard Branson mapema mwezi huu.