Chanzo cha moto sekondari ya Geita chabainika
Jeshi la Polisi mkoa wa Geita limesema chanzo cha matukio ya moto katika shule ya sekondari ya Geita yaliyotokea hivi karibuni ni ugomvi wa muda mrefu kati ya wanafunzi wa kutwa na bweni, ambapo wanafunzi wa kutwa wamedai wanafunzi wa bweni wamekuwa wakipendelewa na uongozi wa shule.