Kocha wa Simba aanza mpango mpya
Kikosi cha mabingwa wa Tanzania bara Simba SC, kimeingia kambini tena hii leo tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kiporo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania, mchezo utakaochezwa Februari 4, 2021, jijini Dodoma. Na kikosi hicho kitaondoka Dar es salaam kesho Feb 3, kuelekea Dodoma.