Manchester City kukaa kileleni EPL leo?
Matajiri wa jiji la Manchester, klabu ya Manchester City itashika usukani wa ligi kuu nchini humo endapo ikifanikiwa kupata ushindi leo Januari 26, 2021saa 5:15 usiku itakapokuwa ugenini kucheza dhidi ya klabu ya West Bromwich Albion.