Watoto wa familia moja wapoteza maisha
Watoto wawili Ashiri Malimi(4) na Laurencia Malimi (2), wakazi wa kata ya Kaseme mkoani Geita, wamefariki dunia huku wengine saba wakinusurika baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba, ulioanguka kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.