Watoto 11 wakamatwa kwa kuiba nyumbani kwa Askari
Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora linawashikilia watoto 11, ambao ni wanafunzi wa shule za msingi kwa tuhuma mbalimbali za uvunjaji, uporaji na unyang’anyi wa kutumia nguvu na silaha katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Tabora mjini na kwamba walivunja nyumba ya Askari mstaafu na kuiba.