Aliyeiibia TANESCO akamatwa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Kagera (TAKUKURU), inatarajia kumfikisha mahakamani mfanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Shamy Magheta, anayetuhumiwa kuomba rushwa ya shilingi 500,000 kutoka kwa mwananchi aliyemlaghai kuwa atampelekea huduma ya umeme.