Majimaji yaweka kando watano kuivaa Yanga
Uongozi wa klabu ya Maji Maji FC ya Songea umewasimamisha wachezaji wake watano kwa tuhuma za utovu wa nidhamu ikiwa ni muda mchache tu kabla ya kucheza mechi yake ya raundi ya 16 kombe la shirikisho dhidi ya Yanga.

