"Mashemeji Derby" yawahamishia wakenya Dar
Fainali ya kwanza ya michuano ya Kombe la SportPesa Super Cup inapigwa leo kwa kuwakutanisha mahasimu AFC Leopards dhidi ya Gor Mahia “Mashemeji Derby” mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

