Stars yaanza vibaya mbio za kuelekea Cameroon
Tanzania usiku wa jana ilianza vibaya mbio za kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon baada ya kukubali sare ya 1-1 dhidi ya Lesotho katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

