Rais Rajoelina ataja sababu za kuikimbia Madagaska
"Nililazimika kutafuta mahali salama pa kulinda maisha yangu," Rajoelina alisema katika hotuba yake ya usiku wa manane, ambayo ilichelewa kwa saa kadhaa baada ya wanajeshi kujaribu kudhibiti majengo ya shirika la utangazaji la serikali, ofisi ya rais ilisema.

