Mbunge ataka wananchi kulinda miradi ya Maendeleo.
Mbunge wa Bahi, Omari Baduwel amewaagiza wakazi wa kata ya Nondwa iliyopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma kuilinda na kuitunza miradi ya maji, barabara na mawasilino iliyopo katika kata hiyo ili iweze kudumu kwani imeigharimu serikali fedha nyingi.