Thursday , 15th Nov , 2018

Spika Mstaafu Pius Msekwa amefunguka juu ya maamuzi ya chama chake kufunga zoezi la kupokea wabunge, madiwani, kuhamia chama hicho na kupewa nafasi ya kugombea tena nafasi zao na kusema yeye anaheshimu maamuzi halali yaliyofanywa na chama chake.

Msemaji wa ACT-Wazalendo Taifa na Spika Mstaafu Pius Msekwa.

Kwa mujibu wa Spika huyo mstaafu kipindi cha utawala wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi amesema maamuzi yoyote yanayofanywa na chama chake ngazi ya  taifa hayawezi kupingwa na mwanachama wa kawaida bali wanapaswa kuyaheshimu kwa kuwa ndiyo msimamo wao.

Msijaribu kushindanisha kipindi hiki na kipindi kile cha serikali ya Rais Mwinyi, kuhusu suala la muda wa mwisho kuhamia CCM sina chochote cha kusema, yale ni maamuzi ya chama, na ninaheshimu maaamuzi ya chama changu,” Spika Mstaafu.

www.eatv.tv pia ilizungumza na Msemaji wa Chama Cha ACT- Wazalendo Taifa Ado Shaibu juu ya siku hiyo ya mwisho kuhamia CCM amesema suala hilo linaonesha fursa mpya kwa wanachama wapya wa CCM na kuonesha taswira kuwa hakuna CCM asilia bali wote ni sawa.

Maoni yangu bunafsi ni ishara ya kufanikiwa kwa makundi ya baadhi ya watu ndani ya CCM wakidai kuwa ni CCM halisi, wakina Nape na viongozi wengine na kuwapa vyeo watu ambao wanajiunga hivi karibuni.”