
Dkt. Charles Tizeba
Dkt. Tizeba ambaye pia ni Mbunge wa Buchosa, alisimama na kupigiwa makofi na wabunge wenzake, kisha akamuomba Naibu Spika kumruhusu kusema maneno mawili tu, na kusema kwamba …. “La kwanza ni kumshukuru sana Mh. Rais kwa Fursa aliyokuwa amenipa ya kulitumikia taifa, lakini pia nikushukuru wewe na Mheshimiwa Spika kwa ushirikiano nilioupata wakati nikitumika serikalini ndani ya Bunge lako”.
Kauli hiyo iliendelea kupigiwa makofi na Wabunge wenzake, na kisha akauliza swali alilokusudia, ambalo lilihusu ujenzi wa vivuko vilivyomo kwenye jimbo lake la Buchosa.
Dkt. Tizeba alikuwa Waziri wa Kilimo ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Magufuli Novemba 10, 2018, kufuatia sakata la ununuzi wa korosho.