Friday , 9th Jun , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amepokea pongezi kutoka kwa Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youging kwa bajet iliyowasilisshwa jana bungeni Mjini Dodoma na waziri wa Fedha kwa kusema imelenga kuongeza maendeleo.

Rais John Pombe Magufuli

Akiwa Ikulu Jijini Dar es salam wakati akifanya mazungumzo na Rais Magufuli , Dkt. Lu Youging amepongeza  bajeti iliyowasilishwa na Waziri Mpango kwa kusema kuwa imeakisi dhamira ya kuongeza kasi ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu na viwanda.

Pamoja na hayo Dkt. Lu Youging amesema kwamba Tanzania ni sehemu ya kipaumbele cha China kwenye suala zima la uwekezaji na kwamba serikali yake itaendelea kushawishi wawekezaji wengi zaidi kuja kuwekeza nchini Tanzania ila kuchangia maendeleo na uzalishaji wa ajira nyingi zaidi.