Wednesday , 26th Mar , 2014

Licha ya kusababisha ajali na madhara makubwa kwa watumiaji wake, biashara ya pikipiki maarufu kama bodaboda imetajwa kuwa suluhisho la ajira kwa idadi kubwa ya vijana nchini Tanzania.

Afisa Miradi mkuu wa taasisi inayojishugulisha na upungzaji ajali ya Amend Bw. Peter Amos, ameiambia East Africa Radio kuwa vijana wengi nchini hivi sasa wameacha vitendo vya uhalifu na badala yake wamejiajiri kwenye biashara ya kubeba abiria kwa kutumia bodaboda.

Amos ameongeza kuwa kuna haja ya vijana hao kutambua umuhimu wa ajira yao kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza wimbi la ajali na vifo vinavyotokana na madereva wa pikipiki hizo kutozingatia sheria za usalama barabarani.