Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza
Akizungumza na Ea Radio Daktari Bingwa wa Magonjwa hayo katika hospitali hiyo ambaye pia ni kiongozi wa zoezi hilo Dk. Charles Kubona amesema kuwa zoezi hilo limesaidia kugundua watu wenye matatizo hayo katika jamii.
Amesema zoezi hilo ambalo limedumu kwa siku tatu ni maandalizi ya madaktari bingwa kutoka mataifa mbalimbali duniani kuja kutoa huduama hiyo kwa wagonjwa kwa muda wa siku tatu.kuanzia Kesho.
Aidha baadhi ya wananchi waliofika kwa ajiri ya uchunguzi wa magonjwa hayo wamepongeza hatua hiyo na kuitaka serikali kuwa na mpango wa kliniki ya huduma hizo kwa wananchi bure kutokana na wengi kuwa na kipato duni.
Msikilize hapa daktari anayesimamia zoezi hilo.



