
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Buguruni Mivinjeni Bw. Barua Mwakilanga ameitaka Serikali kuyaondoa Mabwawa ya maji yaliyopo katika eneo la Sukita huko Buguruni ili eneo hilo litumike kwa ujenzi wa shule za sekondari za kata.
Akizungumza na East Africa Radio leo Bw. Mwakilanga amesema Kata ya Buguruni Mivinjeni haina hata shule moja ya Kata kutokana na kukosekana kwa eneo la kujenga shule hiyo hivyo eneo hilo Sukita ambalo lina mabwawa ya maji ni vyema likatumika kwa ujenzi wa shule hizo.
Bw. Mwakilanga amesema tayari mbunge wa jimbo la Segerea ameshalifikisha bungeni suala hilo na kwamba kinachosubiriwa kwa sasa ni utekelezaji na tayari fedha za ujenzi zilishafanyiwa utaratibu wa kupatikana kutoka kwa wafadhili....