Mbunge wa Kawe Halima Mdee kushoto, Kulia ni Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya
Hukumu hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge, Mhe. George Mkuchika ambaye aliliomba bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao na taarifa ya kamati hiyo ilisema Wabunge Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge.
Hukumu hiyo imeungwa mkono na wabunge wengi waliopitisha azimio hilo ambapo wabunge hao hawataweza kuhudhuria katika vikao vya bunge la saba, nane pamoja na tisa.
Mkuchika amesema kutokana na Kanuni za Bunge hilo zimeweka wazi adhabu ya mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20.
