
Dkt Reginald Mengi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP
Dk. Mengi ametoa wito huo wakati akiwazawadia waandishi wa Makapuni ya IPP walioshiriki na kushinda Tuzo za Umahiri katika Uandishi wa Habari (EJAT) za mwaka 2013 zilizotolewa na Baraza la Habari Tanzania—MCT.
Akiongea na waandishi hao baada ya kuwakabidhi zawadi zao katika hafla iliyohudhuriwa na wakurugenzi na wahariri wa vyombo hivyo, Dkt Mengi amewataka waandishi hao kuandika kwa niaba ya wale wasiokuwa na sauti au majukwaa ya kupaza sauti zao ili sauti zao zisikike.
Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, baadhi ya waandishi hao ambao ni kutoka vyombo vya ITV/Radio One na magazeti ya The Guardian na Nipashe, wameeleza furaha yao hasa kazi zao zinapotambuliwa na kutunzwa pamoja na kutiwa moyo na viongozi wao.