Akiongea na East Africa Radio katika mahojiano maalumu jijini Dar es salaam,Rais wa chama cha mawakala wa forodha nchini TAFA Bwana Steven Ngatunga amesema, wafanyabiashara wengi hupata hasara na kuingia garama zisizo zalazima kutokana na kutokuwa na nyarama muhimu.
Bwana Ngatunga amesema, ili kuepuka usumbufu hasa kwa wafanyabiashara kutoka nje ya nchi ni vyema kuonana na wakala wa forodha aliyesajiliwa kuweza kupata msaada wiki mbili kabla ya meli yamizigo kuwasili bandarini hapo.