Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage, wakati akizungumza na wataalam wa magonjwa hayo na wadau wakuhamasisha mapambano dhidi ya saratani kutoka nchi mbalimbali.
Amesema kwa sasa saratani ya kizazi na saratani ya matiti ndizo zinaongoza kuwa na wagonjwa wengi zaidi kutokana na mfumo wa maisha ulivyo na kuongeza kuwa huduma za Saratani haziwezi kuimarishwa na serikali pekee lazima kuwe na ushirikiano na wadau wote wa afya.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Hospitali ya Agha Khan, Dkt. Omary Sherman amesema Saratan, ya matiti inaenea kwa kasi bila wahusika kujua.