Wednesday , 14th Dec , 2016

Timu tisa kutoka Uganda, Tanzania Bara na wenyeji Zanzibar zinatarajiwa kushiriki katika Mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) yanayotarajiwa kutimua vumbi kuanzia Desemba 30 mwaka huu.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Omar Hassan Omar ‘King’ amesema, mashindano hayo yatasimamiwa na Kamati maalumu ambayo imechaguliwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA).

Omar amesema, mashindano hayo yatasimamiwa na Sharifa Khamis ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati huku katibu wa Kamati hiyo akiwa ni Khamis Abdalla Said.

Wajumbe wa Kamati ni Ali Khalil Mirza, Khamis Mzee Ali, Juma Mmanga, Ravia Idarous Faina, Mohammed Ali, Mohammed Ali Hilal, Issa Mlingoti Ali, Dk. Ally Saleh Mwinyikai na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Omar Hassan Omar ‘King’.