Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa ameeleza kuwa kata ya Pemba Mnazi imekuwa uchochoro wa kupitisha bidhaa za magendo kitendo kinachoikosesha mapato wilaya yake na serikali kuu kwa ujumla hivyo ni lazima hali hiyo idhibitiwe haraka.
Mhe. Mgandilwa amesema, uhalifu pia umekithiri zaidi katani humo na kwamba askari wataongezwa kuweza kukabiliana na hali hiyo na kuwaweka wananchi kwenye mazingira ya usalama wao na mali zao
Kigamboni ni miongoni mwa wilaya mpya iliyotokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Temeke, Wilaya hiyo ya Kigamboni ina kilometa za mraba 416 ikiwa na kata 9, mitaa 67 na tarafa 01 huku idadi ya watu ikiwa ni laki moja na tisini na tano elfu.