Monday , 31st Oct , 2016

Serikali ya Kenya imetoa shilingi bilioni 5 za nchi hiyo ili kukabiliana na ukame uliopo hivi sasa katika maeneo tofauti ya nchi hiyo, Waziri wa Ugatuzi na Mipango Mwangi Kiunjuri amesema.

Waziri wa Ugatuzi na Mipango, Mwangi Kiunjuri.

 

Waziri Kiunjuri ametoa kauli hiyo wakati alipoambatana na Kamati ya Bunge ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi katika kaunti ya Samburu kutathimini athari za kiuchumi kwa wafugaji hao kutokana na ukame.

Kutoka katika fedha hizo shilingi bilioni 1.2 za Kenya zitatumika kununua mifugo kutoka kwa wafugaji kwenye maeneo yaliyoathiriwa na ukame, kazi ambayo mchakato wake umeanza.