
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam Lazaro Mambosasa.
Mambosasa ameyasema hayo leo Desemba 31, 2018, Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa jeshi hilo na mafanikio yake katika kipindi cha mwaka mmoja.
"Kipindi cha mwaka mmoja fedha tulizofanikiwa kukusanya ni bilioni 29, kwa watuhumiwa wa makosa ya kukamatwa kwa vyombo vya usafiri na wenyewe wakakiri kufanya makosa hayo".
Aidha Kamanda Mambosasa ameogeza, "naomba wadau tushirikiane kwa pamoja kuhusu wahamiaji haramu, kwa hapa DSM kuna wimbi kubwa la matapeli ambao ni raia wa kigeni na wanafanya uhalifu, hili eneo si la kufumbiwa macho, unakuta mstaafu katoka kuchukua kiinua mgongo, anatapeliwa".
"Wanachi wanaumizwa kweli mmoja hapo chini kuna mstaafu ametapeliwa milioni 120, na mnigeria ambaye ameingia nchini na anaishi bila kibali."
Katika hatua nyingine Kamanda Mambosasa amewaonya wananchi watakaosherehekea mkesha wa mwaka mpya kwa kufyatua mafataki badala yake ametoa dakika 5 kwa watakaotaka kufanya tukio hilo kuanzia saa 6 kamili usiku hadi saa 6.05 usiku.