
Abdallah Mtolea, Mbunge mteule wa jimbo la Temeke.
Akitangaza ushindi huo Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi, amesema Mtolea ameshinda kiti hicho cha Ubunge baada ya wagombea wengine kushindwa kutimiza vigezo vya kugombea ikiwemo kukosea kujaza fomu.
"Abdallah Mtolea mgombea wa CCM, ameteuliwa kwakuwa ametimiza masharti yote kama kanuni zinavyoelekeza, na kwa mamlaka niliyopewa kwa mujibu wa sheria namtangaza ndugu Mtolea kuwa Mbunge mteule wa jimbo la Temeke", amesema Mwakabibi.
Mtolea alitangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo na kisha kukihama chama chake cha CUF na kujiunga na CCM, ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM), kilimpa nafasi ya kugombea Ubunge kwenye jimbo hilo kwa mara nyingine.