Monday , 31st Oct , 2016

Takwimu zinaonesha kuwa watoto wengi wenye matatizo ya usonji wanaongezeka kwa kukaa majumbani kutegemea ulezi wa wazazi kutokana na kukosa elimu huku ikielezwa elimu wanayoipata ni ile ya awali na msingi pekee.

Baadhi ya watoto wenye matatizo usonji

 

Akizungumza jijini Arusha na wadau wa watoto wa usonji yaani watoto wenye ulemavu wa akili mkurugenzi wa taasisi inayoshughulika na watoto hao Bi. Graciana Lyimo amesema ipo haja ya mfumo wa elimu wa kundi hilo ukatazamwa upya.

Bi. Lyimo amesema kuwa serikali bado haijakuwa na mpango maalum wa kuweza kuandaa mazingira ya kitu kingine cha ziada wanachoweza kufanya mara baada ya kumaliza elimu ya msingi hali inayowafanya kuendelea kuwa tegemezi majumbani.

Naye Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha walemavu kupitia Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Elly Macha ameitaka serika kuanzisha vyuo vya ufundi kwa watu hao ili kuwaondoa kwenye utegemezi zaidi.