
Baadhi ya wanafunzi nchini Tanzania
Akizungumza na East Africa Radio kwa niaba ya mkuu wa shule hiyo, katika semina ya ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma PETS, ilyoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la TALIA, mwalimu Mariam Bakili amesema kuwa wanafunzi watatu wameachishwa masomo kwa mwaka huu kutokana na tatizo hilo.
Aidha, Mkuu wa Milaya ya Masasi Seleman Mzee, akihitimisha semina hiyo, amewataka walimu na watendaji wa kata kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria masomo, huku mwezeshaji katika semina hiyo, Liliane Mgaya, akieleza faida za semina kwa washiriki
Serikali inatoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 21 kila mwezi ambazo zinaekelezwa katika mpango wa elimu bila malipo.