Wanafunzi wakiwa katika chumba cha mtihani
Akitoa taarifa ya kuanza kwa mtihani huo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania, Dkt. Charles Msonde, amesema maandalizi yote ya kufanyika kwa mtihani huo yamekamilika huku akitoa onyo kwa watakaojaribu kufanya udanganyifu katika mitihani hiyo.
Dkt. Msonde amesema matokeo ya mtihani huo yatatumika katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na elimu ya juu ya kidato cha tano, kupata wataaluma wa fani mbalimbali kama vile afya, kilimo, ualimu na ufundi.





