Friday , 4th Nov , 2016

Msanii kutoka kundi la Wagosi wa Kaya maarufu kwa jina la MKOLONI amewasihi wasanii wa sasa kuimba ukweli katika nyimbo zao ili kuelimisha jamii uhalisia wa maisha yaliyopo.

Mkoloni

 

Akipiga story ndani ya eNewz Mkoloni amesema haoni sababu ya wasanii wa sasa kuimba starehe na kuonesha maisha ni rahisi hali inayopotosha jamii wakati kuna watu wanateseka na hawana hata makazi maalum ya kuishi.

Hata hivyo Mkoloni amewataka wasanii kuimba nyimbo za kuelimisha kama walivyokuwa wanaimba zamani ili kuweza kuiweka jamii sawa na siyo kuimba mambo ambayo ukiyasikia mpaka unashangaa wakati anapokaa huyo msanii akipita ni lazima avue viatu kwa kuwa kuna matope sana.