Thursday , 15th Jun , 2017

Serikali imelifungia gazeti la Mawio kwa miezi 24, kwa kuwahusisha marasi wastaafu Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete sakata la mchanga wa madini (Makanikia).

Barua kutoka kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Harrison Mwakwembe kwenda kwa Mhariri Mkuu wa gazeti hilo inasema kwamba licha gazeti hilo kukiuka maagizo ya serikali lakini pia imekiuka vifungu vinavyokataza uandishi hasi. 

Aidha barua hiyo imekanusha Marais tajwa kuhusika na sakata la mchanga na kwamba hawakuwa kwenye sehemu ya uchunguzi ya Kamati za Rais na matokeo ya kamati hizo hayajawatuhumu kwa kosa lolote.